Kuchanganya nguo zilizoingiwa na mate ya mbwa na nguo zengine

Swali: Ni ipi hukumu ya mate ya mbwa yanapoingia kwenye mwili wa mtu na yanapoingia nguoni? Ni ipi hukumu ya nguo inayooshwa na nguo hiyo katika mashine moja na maji hayohayo?

Jibu: Mate ya mbwa ni najisi na ni lazima kuosha kile chombo au nguo iliyoguswa na mate yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kukitwahirisha chombo cha mmoja wenu anapokiramba mbwa anakiosha mara saba, muosho wa kwanza kwa mchanga.”

Nguo zinapowekwa ndani ya maji masafi na zikaoshwa mpaka ikaondoka ile athari ya najisi husafika zote kutokana na ile najisi ya mbwa na uchafu mwingine. Kwa sharti zioshwe mara saba kutokana na najisi ya mbwa ambapo muosho wa kwanza uwe kwa mchanga au vile vinavyokaa mahali pake kama sabuni au Ashnaan[1].

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Saltwort

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (04/196) nr. (17558)
  • Imechapishwa: 06/06/2022