Swali: Baadhi ya wanawake hubadilisha nywele kuwa rangi nyekundu.

Jibu: Hapana vibaya. Rangi nyekundu haina neno. Kilichokatazwa ni rangi nyeusi. Lakini kuzibadilisha kwa rangi nyekundu, rangi ilio kati ya nyekundu na nyeusi au kwa shakili ya manjano haina vibaya.

Swali: Ikiwa makusudio yao ni mtindo?

Jibu: Muhimu abadilishe mvi kwa rangi isiyokuwa nyeusi. Hakuna vibaya kwa lengo lolote. Hata hivyo jambo hilo lisiwe na kujifananisha. Ikiwa ni jambo maalum kwa makafiri wa kike haitojuzu kwao kufanya hivo.

Swali: Ikiwa ni kwa lengo la mtindo kunaingia katika kujifananisha na makafiri?

Jibu: Akiwa katika nchi ya makafiri asijifananishe nao. Ama ikiwa waislamu wa mji wake wanafanya jambo hilo; rangi ya manjano, nyekundu au akaona kuwa rangi hiyo inampendeza zaidi na asikusudie kujifananisha, ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21936/حكم-تغيير-لون-الشعر-الى-الاحمر-او-غيره
  • Imechapishwa: 12/01/2023