Swali: Baadhi ya watu ukiwaapia kwa jina la Allaah wanakataa na wanataka uape kwa msahafu na hawakuoni ni mkweli mpaka uape kwa msahafu.

Jibu: Hapana, hakuhitajiki kuapa kwa msahafu. Hakuna haja ya kuwakalifisha watu. Hiyo ni njia moja wapo ya kukifanya kikubwa kiapo. Si lazima kufanya hivo. Inatosha kuapa kwa jina la Allaah tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22064/ما-حكم-الحلف-على-المصحف
  • Imechapishwa: 21/10/2022