Swali: Kuna mwanamke ameporomosha mimba baada ya kukamilika kwake.

Jibu: Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah na ni lazima kwake kutoa diyaa. Vilevile anatakiwa kuadhibiwa na kutiwa adabu.

Swali: Hana kafara?

Jibu: Hapana. Ikiwa amefanya hivo kwa makusudi hakuna kafara. Kafara inakuwa kuua kimakosa au tukio linalofanana na kuua kimakosa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22066/حكم-من-اسقطت-جنينها-متعمدة-بعد-اكتماله
  • Imechapishwa: 21/10/2022