Swali: Kuacha swalah ya Fajr [msikitini] ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa?

Jibu: Ikiwa amekosa swalah ya Fajr lakini ameswali ndani ya wakati ni maasi. Na ikiwa amekosa mpaka ukatoka wakati wake ni ukafiri na sio Bid´ah. Ni miongoni mwa mambo ya ukafiri. Kuacha swalah ya mkusanyiko ni maasi. Kuiacha ikatoka nje ya wakati wake ni ukafiri. Tunamuomba Allaah afya.

Bid´ah maana yake ni kuzua Shari´ah mpya ndani ya dini. Hii ndio Bid´ah. Kule kuzua kwake kitu na akaona kuwa kumewekwa katika Shari´ah ilihali Allaah hakukiweka ndio huitwa Bid´ah. Lakini akifanya kitu cha maovu inaitwa kuwa ni maasi na haiitwi kuwa ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21525/ما-حكم-التخلف-عن-صلاة-الفجر
  • Imechapishwa: 25/08/2022