Swali: Imepokelewa katika Hadiyth:

“Atakayekaa katika mkeka wake baada ya swalah ya Fajr mpaka jua kuchomoza ni kama ambaye amefanya Hajj na ´Umrah kikamilifu kikamilifu.”

au maneno mfano wa hayo. Je, hiyo ina maana kwamba mwenye kufanya hivo ana ujira mfano wa yule aliyefanya Hajj na ´Umrah au ni vipi?

Jibu: Mosi: Hadiyth hii kuna maneno juu yake. Wanachuoni wengi wameidhoofisha.

Pili: Tukichukulia kuwa ni Swahiyh thawabu hazitakiwi kufanyiwa kipimo. Mtu anaweza kulipwa kwa kitendo kidogo thawabu za matendo mengi. Kwa sababu thawabu ni fadhilah kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) anazompa amtakaye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1737
  • Imechapishwa: 25/09/2020