Kisomo cha kwa pamoja kabla ya Khutbah ya ijumaa

Swali: Katika baadhi ya miji ya kiarabu baadhi wanasoma Suurah moja wapo kwenye Qur-aan kwa njia ya pamoja kabla ya Khutbah ya ijumaa. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kusoma kwa njia kama hii ni Bid´ah. Kisomo cha pamoja ni Bid´ah ikiwa malengo sio kwa ajili ya kujifunza. Ni sawa kwa mwalimu kusoma Aayah moja na wanafunzi wakairudilia kwa lengo la kujifunza, lakini hapana iwapo lengo itakuwa ni kwa ajili ya kusoma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017