Kimsingi ni kunyanyua mikono wakati wa du´aa

Swali: Ni kipi kigezo juu ya kunyanyua mikono kwa ajili ya du´aa? Ni lini tunaruhusiwa kunyanyua mikono na lini haturuhusiwi kunyanyua?

Jibu: Sehemu ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba du´aa na hakunyanyua mikono yake, na sisi pia haifai kunyanyua. Mbali na sehemu hizi, asli ni kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa. Kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa ni katika sababu za kuitikiwa. Lakini sehemu ambazo imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameomba du´aa na hakunyanyua mikono yake, na sisi hatunyanyui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020