Swali: Walii anakuwa na karama zenye kuthibitisha kuwa kweli ni katika mawalii wa Allaah? Je, inajuzu kuziweka wazi karama hizi?

Jibu: Sio lazima walii awe na karama. Kuna uwezekano akawa nazo na kuna uwezekano vilevile asiwe nazo. Kuna ambao ni mawalii wakubwa na hawana karama. Karama wakati mwingine zinakuja kutokana na waislamu kuzihitajia au kwa ajili ya kusimamisha hoja katika dini. Zinakuja wakati wa haja tu. Sio lazima kila walii kudhihirike kwake karama. Hili sio lazima. Haijuzu kwa yule ambaye kumedhihiri kwake kitu kukielezea, kujifakhari kwa hilo na akajiona. Kinyume chake yanatakiwa kumzidishia unyenyekevu. Karama zinatakiwa kumzidishia karama na kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 22/10/2016