Kila sifa ya ukanushaji inathibitisha ukamilifu wa kinyume chake

Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hashindwi na jambo.”

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Ahl-ul-Haqq wanaamini ya kwamba Allaah hashindwi na jambo kutokana na ukamilifu wa uwezo Wake. Allaah (Ta´ala) Amesema:

إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Allaah anaumba atakavyo. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.” (24:45)

وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا

“Na Allaah daima juu ya kila kitu ni Mweza.” (18:45)

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا

“Na hakuna lolote lile limshindalo Allaah mbinguni na wala ardhini. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.” (35:44)

Makanusho haya yanalazimisha kuthibitisha kinyume chake ambako ni ukamilifu. Kila ukanushaji uliothibiti katika Qur-aan na Sunanh juu ya haki ya Allaah (´Azza wa Jall) inatakikana kuthibitisha kinyume chake ambako ni ukamilifu. Kwa ajili hiyo ndio maana Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ

“Na hakuna lolote lile limshindalo Allaah.” (35:44)

Kisha Akasema:

إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا

“Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hekima.” (04:11)

Huu ni ukanushaji.

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ

“Na hakuna lolote lile limshindalo Allaah.” (35:44)

Kutokana na ukamilifu wa ujuzi Wake na uwezo Wake.

Vilevile kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا

“Na Mola wako Hamdhulumu yeyote.” (18:49)

Amekanusha dhuluma na kuna uthibitishaji wa ukamilifu wa kinyume chake:

لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ

“Hakifichiki Kwake chochote [hata kiwe] uzito wa atomu mbinguni wala ardhini.” (34:03)

Kutokana na ukamilifu wa ujuzi Wake.

وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا

“Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo [mbingu na ardh].” (02:255)

Kutokana na ukamilifu wa uwezo Wake.

لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ

“Haumchukuwi usingizi wala kulala.” (02:255)

Kutokana na ukamilifu wa uhai Wake.

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki bali Yeye anayazunguka macho yote.” (06:103)

Kutokana na ukamilifu wa ukubwa Wake na Utukufu Wake.

Hali kadhalika kila sifa inayokuja katika Qur-aan na Sunnah inayokunusha inathibitisha ukamilifu wa kinyume chake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/40-41)
  • Imechapishwa: 07/06/2020