Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah):

“Hakuna awezae kumwaza wala kufahamu dhati Yake.”

Maana yake ni kwamba hakuna awezae kumwaza na kumjua. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) fahamu haziwezi kumtambua wala kumzunguka kwa ujuzi. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“… na wala hawawezi kuizunguka elimu Yake.” (20:110)

Viumbe hawawezi kumjua Yuko namna gani na uhakika Wake. Wanaweza kumtambua kwa Majina na sifa Zake. Watamuona siku ya Qiyaamah [pasina kumzunguka wote]. Hii ni dalili inayoonesha ukamilifu wa ukubwa Wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/61)
  • Imechapishwa: 07/06/2020