Kila mmoja ataridhika na alichonacho Peponi

Swali: Ni jambo linalojulikana ya kwamba waumini Peponi wanatofautiana katika fadhila. Vipi tutaoanisha hili na kwamba muumini atapata kila ambacho anakitamani Peponi? Je, akitamani daraja ya ambaye yuko juu yake ataipata?

Jibu: Hapana, hawezi kuipata. Lakini hata hivyo haoni kama kuna ambaye ana furaha kama yeye. Allaah ataweka ndani ya nafsi yake raha na ukinaikaji na neema mpaka aone kuwa hakuna ambaye ana mazuri kumshinda. Peponi hakuna hasadi wala chuki. Kila mmoja atakuwa ni mwenye kufurahikia yale aliyomo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-25.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020