Haijuzu kuleta Basmalah kabla ya kusoma Suurat-ut-Tawbah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuleta Basmalah mwanzoni wa Suurat-ut-Tawbah?

Jibu: Haijuzu. Haijuzu kuleta Basmalah mwanzoni wa Suurat-ut-Tawbah. Kwa kuwa haikuteremshwa kabla yake. Hivyo mtu asisemi “Bismillaahi Rahmaani Rahiym” mwanzoni wa Suurat-ut-Tawbah. Haikuandikwa kwenye misahafu na [Basmalah] haikuandikwa kabla yake kama zilivyo Suurah zingine. Atakuwa ni mwenye kuzidisha katika Suurat-ut-Tawbah. Akiileta kabla ya Suurah at-Tawbah atahesabika amezidisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-25.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020