al-Fawzaan kusoma kiarabu kwa Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Sijapata yeyote wa kunifunza lugha ya kiarabu isipokuwa mtu ambaye ametahadharishwa na baadhi ya wanafunzi wakubwa kutokana na ´Aqiydah yake na wamesema kuwa nisome lugha kwa watu wenye mfumo wa Salaf hata kama nitachelewa sana kusoma kwa kuwa wengi katika watu hawa ni Ashaa´irah. Je, nisome elimu ya kiarabu kwa mtu huyu au nisifanye hivo?

Jibu: Wanaofunza lugha ya kiarabu ni wengi na himdi zote ni za Allaah. Wanaofunza sarafu ni wengi. Soma kwa mtu anayefunza sarafu ambaye ana ´Aqiydah iliosalimika. Utampata – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-25.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020