Swali: Nifanye nini ikiwa nimepewa mtihani kwa dhambi na nikawa naificha kwa watu na kila ninapotubu hurudi kuifanya, bi maana natubu na kurudi tena. Pamoja na kwamba huazimia kudumu na sifanyi hivo kwa matamanio, bali ni mtego wa Shaytwaan na humuomba Allaah aniokoe nayo.
Jibu: Endelea kufanya hivi. Ni juu yako kutodhirisha maasi. Unapopewa mtihani jifiche na usionyeshe hadharani. Wakati huo huo kuwa ni mwenye kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hata kama kufanya hivi kutakariri kwako usife moyo na Rahmah za Allaah. Endelea kutubu kwa Allaah. Kila mara tubu kwa Allaah. Allaah Humsamehe mwenye kutubia. Usikate tamaa na Rahmah za Allaah. Vilevile usikate tamaa na kuacha maasi. Inawezekana kukaja wakati ambapo ukayaacha kwa kule kuomba sana Tawbah. Hili ni mosi.
Pili ni kwamba, sio sharti kwa yule anayeamrisha mema na kukataza maovu awe hakosei. Sisi wote tuna madhambi. Sisi wote tuna mapungufu. Lakini hayo yawe yameambatana na kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kuwa na khofu kwa Allaah (´Azza wa Jall).
Tunaamrisha mema na kukataza maovu hata kama tutakuwa na kasoro. Hatukusanyi kati ya kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu katika hali hiyo tuwe tumekusanya kati ya jarima mbili.
Baadhi ya watu wanasema kuwa hawaamrishi mema na kukataza maovu kwa sababu mimi mwenyewe nafanya mambo haya. Hapana. Hilo halikatiki juu yako. Kuamrisha mema na kukataza maovu bado liko juu yako hata kama wewe mwenyewe utakuwa unayafanya. Ukiyafanya tubu kwa Allaah. Mlango wa Tawbah uko wazi. Hukufungiwa nao. Usiache kuamrisha mema na kukataza maovu kwani katika hali hiyo utakuwa umekusanya kati ya jarima mbili; kwenda kinyume na kuacha jambo ambalo ni la wajibu.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%204-13-08-1433.mp3
- Imechapishwa: 16/06/2015
Swali: Nifanye nini ikiwa nimepewa mtihani kwa dhambi na nikawa naificha kwa watu na kila ninapotubu hurudi kuifanya, bi maana natubu na kurudi tena. Pamoja na kwamba huazimia kudumu na sifanyi hivo kwa matamanio, bali ni mtego wa Shaytwaan na humuomba Allaah aniokoe nayo.
Jibu: Endelea kufanya hivi. Ni juu yako kutodhirisha maasi. Unapopewa mtihani jifiche na usionyeshe hadharani. Wakati huo huo kuwa ni mwenye kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hata kama kufanya hivi kutakariri kwako usife moyo na Rahmah za Allaah. Endelea kutubu kwa Allaah. Kila mara tubu kwa Allaah. Allaah Humsamehe mwenye kutubia. Usikate tamaa na Rahmah za Allaah. Vilevile usikate tamaa na kuacha maasi. Inawezekana kukaja wakati ambapo ukayaacha kwa kule kuomba sana Tawbah. Hili ni mosi.
Pili ni kwamba, sio sharti kwa yule anayeamrisha mema na kukataza maovu awe hakosei. Sisi wote tuna madhambi. Sisi wote tuna mapungufu. Lakini hayo yawe yameambatana na kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kuwa na khofu kwa Allaah (´Azza wa Jall).
Tunaamrisha mema na kukataza maovu hata kama tutakuwa na kasoro. Hatukusanyi kati ya kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu katika hali hiyo tuwe tumekusanya kati ya jarima mbili.
Baadhi ya watu wanasema kuwa hawaamrishi mema na kukataza maovu kwa sababu mimi mwenyewe nafanya mambo haya. Hapana. Hilo halikatiki juu yako. Kuamrisha mema na kukataza maovu bado liko juu yako hata kama wewe mwenyewe utakuwa unayafanya. Ukiyafanya tubu kwa Allaah. Mlango wa Tawbah uko wazi. Hukufungiwa nao. Usiache kuamrisha mema na kukataza maovu kwani katika hali hiyo utakuwa umekusanya kati ya jarima mbili; kwenda kinyume na kuacha jambo ambalo ni la wajibu.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%204-13-08-1433.mp3
Imechapishwa: 16/06/2015
https://firqatunnajia.com/kila-anapotubu-kwa-dhambi-anarudi-tena-kuifanya/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)