608- Nilimsikia Ahmad akiulizwa ni kina nani ambao mtu anatakiwa kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr. Akajibu:

“Kila ambaye anawajibika kumhudumia.”

Kukasemwa: “Vipi ikiwa mwanamme anamlea msichana ambaye amefiwa na baba yake?” Akajibu:

“Basi atatakiwa kumtolea yeye pia.”

Nikasema: “Je, awatolee ndugu zake anaowahudumia?” Akajibu:

“Nimeshajibu swali lako. Amtolee kila ambaye anamuhudumia.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 125
  • Imechapishwa: 20/03/2021