38. Kikosi cha wasafiri wanatakiwa kuswali mkusanyiko


Swali 38: Mtu akisafiri kutoka Riyaadh kwenda Makkah na akiwa njiani atapitia Qaswiym na hapo wapo baadhi ya jamaa zake ambapo akakaa nyumbani kwao siku mbili – je, atazingatiwa kuwa ni msafiri au mkazi[1]?

Jibu: Huyu anazingatiwa ni msafiri maadamu hayuko katika mji wake ijapo atakuwa na jamaa zake, kama vile kaka, dada au wengineo. Lakini asiswali peke yake. Aswali na mkusanyiko na akamilishe pamoja nao Rak´ah nne kwa sababu inamlazimu swalah ya mkusanyiko. Lakini akiwa na mtu au watu wengine pamoja naye basi itafaa kwao kuswali kwa kufupisha. Vilevile inafaa kwao kuswali pamoja na mkusanyiko wa mji na wakamilishe. Ama akinuia kukaa zaidi ya siku nne, basi analazimika kukamilisha zile swalah za Rak´ah nnenne. Ni mamoja msafiri atakuwa peke yake au watakuwa kikundi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/299).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 54
  • Imechapishwa: 15/05/2022