39. Swalah ya ´iyd mashambani


Swali 39: Siku moja nilienda shambani nchini mwangu Afrika na ikaangukia kwamba nimefika siku ya ´Iyd-ul-Adhwhaa ambapo nikawaona watu – waume kwa wake – wanakimbilia makaburini kwa ajili ya kuyatembelea makaburi. Asubuhi ya siku ya ´iyd akatunzwa kila ambaye amehudhuria swalah makaburini. Walikuwa wametanguliwa na mzee ambaye akawaswalisha wote isipokuwa mimi ambaye nilibaki hali ya kuchanganyikiwa na kustaajabu kwa yale niliyoyaona na sikuswali pamoja nao swalah hiyo waliyoiita kuwa ni swalah ya ´iyd. Ni ipi hukumu ya Uislamu juu ya swalah hiyo pamoja na kuzingatia kwamba watu wa mashambani ambao nawakusudia hawana msikiti? Wanaishi ndani ya mahema baadhi wakiwa mbali na wengine. Angalizo! Ninaposema kuwa wanaswali makaburini nakusudia pambizoni mwake wakiwa mbali kabisa na makaburi[1].

Jibu: Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.

Swalah ya ´iyd inaswaliwa katika miji. Haikuwekwa katika Shari´ah kuisimamisha majangwani na safarini. Hivo ndivo ilivyopokea Sunnah kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haikuhifadhiwa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba waliswali swalah ya ´iyd safarini wala shambani.

Alihiji hijjah ya kuaga (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hakuswali swalah ya ijumaa ´Arafah. Siku hiyo ilikuwa siku ya ijumaa. Wala hakuswali swalah ya ´iyd Minaa. Kila kheri na furaha inapatikana kwa kumfuata yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/08-09).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 15/05/2022