Kigezo kwa wanawake wanapopiga dufu

Swali: Ni kipi kidhibiti katika sherehe za wanawake pindi wanapopiga dufu?

Jibu: Kidhibiti ni kwamba pale wanapokusanyika sehemu ambapo kumejificha na wakawa wenyewe ule usiku wa ndoa ni sawa wakapiga dufu. Wapige dufu bila ya mafilimbi. Wapige dufu zinazojulikana kupigwa kwa mkono. Sauti zao zisisikike na wanaume nje. Wasipige dufu kwa kutumia vipaza sauti au mkanda. Kusiwepo mambo kama haya. Pindi wanapokusanyika malengo iwe ni kuitangaza ndoa tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-07.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020