Huyu sio mtafutaji elimu – huyu ni mtafutaji fitina!

Swali: Ni ipi hukumu kwa anayejinasibisha na kutafuta elimu na anatafuta fataawaa mbovu zinazoenda kinyume na wanachuoni?

Jibu: Huyu sio mtafutaji wa elimu. Huyu ni mtafutaji wa fitina. Huyu ni mtafutaji wa fitina na wala hatumwiti kuwa ni mtafutaji wa elimu. Mtafuta elimu ni yule anayetafiti haki. Huyu ndiye mtafutaji elimu. Ni yule anayetafiti haki na dalili. Ama yule anayepekua fataawaa mbovu na maneno ya tofauti, huyu tunasema kuwa ni mtafutaji wa fitina na sio mtafutaji wa elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-07.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020