Swali: Tunaomba utuwekee wazi hukumu ya Kishari´ah juu ya kunyoa ndevu na ni lini mtu anakuwa ni mwenye kutenzwa nguvu kuzinyoa ikiwa anakabiliwa na changamoto kwenye mji wake?

Jibu: Asubiri juu ya Dini yake na ndevu. Asiache kitu katika Dini yake hata kama atakabiliwa na maudhi ya hali ya juu. Hakuna dharurah kamwe ya kunyoa ndevu. Hakuna dharurah. Ni kweli kuna maudhi. Lakini hata hivyo kuwa ni mwenye subira. Dharurah ni kama wataka kuuawa; ima nyoa ndevu zako au tunakuua au wakakunyoa nazo kwa nguvu. Huku ndio kutenzwa nguvu au dharurah. Ama kusema tu kuwa unanyanyaswa na kuudhiwa, kuwa ni mwenye subira juu ya haya. Wewe uko juu ya haki na wao wako katika batili. Usiwanyenyekei.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-07.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020