Haifai kufanya kazi kwenye mgahawa mchana wa Ramadhaan

Swali: Nafanya kazi kwenye mgahawa Ufaransa. Je, inajuzu kwangu kuuza chakula mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Hapana, huku ni kushirikiana katika dhambi na uadui. Usiuze chakula nchana wa Ramadhaan ilihali wewe ni muislamu. Kufanya hivi ni kushirikiana katika dhambi na uadui. Usifanye kazi katika mgahawa huu mchana wa Ramadhaan. Unaweza kufanya kazi usiku au nje [ya mwezi wa] Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-07.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020