Kigezo cha kuonyesha neema za Allaah

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah anapenda kuona athari ya neema Zake kwa mja.”

Kuna kigezo gani cha kuonekana athari ya neema kwa mja?

Jibu: Katika chakula na kinywaji chake. Asivae kama wanavyovaa mafukara. Ni aina fulani ya ubakhili na kukanusha neema.

Swali: Mfanyabiashara ambaye kipato chake kimekuwa ni kumi…

Jibu: Tunachokusudia ni kwamba ale, anywe na avae mavazi ya matajiri wenzake. Lengo ni ili asikanushe neema za Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23320/ما-الضابط-في-اظهار-اثر-النعمة
  • Imechapishwa: 23/12/2023