Kidhibiti cha mwanamme kusaidia kazi za nyumbani

Amesema (Ta´ala):

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Nao wake wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa wema; na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[1]

وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ

“Na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[2]

Hakuna usawa kati ya mwanaume na mwanamke isipokuwa katika yale hekima inapelekea kuwa na usawa. Nasema kwamba hili linategemea na desturi. Ikiwa desturi mke ndiye anamhudumia mume wake katika hazina, kupika, kufua na kutengeneza shamba hakuna neno. Mke wa az-Zubayr bin al-´Awaam yeye ndiye alikuwa akipeleka mizigo kutoka al-Madiynah hadi nyumbani kwake nje ya al-Madiynah. Huyu alikuwa ni mke wake. Watu katika wakati wetu huu ambao tumekutana nao mwanamke ndiye ambaye anatengeneza nyumba, kufanya usafi, kuosha vyombo, kuwakamua ng´ombe maziwa, kupika na mengineyo yote. Mwanamume jukumu lake ni kuleta matumizi. Kimsingi mambo ni hivi. Lakini hapana neno mume kumsaidia mke wake kwa ajili ya kumuheshimisha na kujiweka karibu naye. Haya yana manufaa makubwa.

Kuhusu yale aliyofikiria muulizaji ya kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), mama wa waumini, alikuwa akilala zake na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye ndiye ambaye anapambana na kupika, ni uongo na si khabari za kweli. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akija na akikuta chakula chake kimeshaandaliwa na wakati mwingine anakuja na kuuliza kama kuna chakula. Kuna wakati alikuja akakuta chungu kiko juu ya moto wanapika nyama na akauliza juu yake. Lakini hapana shaka kwamba alikuwa akisaidia familia yake. Hapana shaka kwamba alikuwa akishona viatu vyake na akikausha nguo zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini kuyafanya mambo yaonekane kama alivyofikiria mtu huyu… ima ni mjinga au mambo yamefichikana kwake. Kwa hali yoyote Uislamu umesema:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Kaeni nao kwa wema.”[3]

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ

 “Nao wake wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa wema; na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[4]

Kwa hivyo mtu anatakiwa kufuata desturi. Huenda desturi hii leo imetofautiana na hali ilivyokuwa hapo kale. Hapo kabla mwanamke alikuwa ndiye anajitwisha kazi zote za  nyumbani. Sisi tulikutana na makubwa kuliko yaliyoko hii leo. Leo mwanamke amekuwa anaweza kuomba mfanyikazi, anaweza kumwambia mume wake pindi wanapotoka wote wawili kwenda sokoni kwamba yeye ndiye abebe mtoto na yeye amfuate na wakati mwingine anamwambia ambebe mtoto na yeye amfuate nyuma yake. Haya ni mambo yako. Lakini huku ni kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake? Hapana. Ni kuwaiga jamii za kimagharibi. Kwa ajili hiyo ndio maana tunatakiwa kushikamana na mila zetu midhali hatujaona mila ambayo ni bora kuliko yetu kwa njia ya Shari´ah. Mimi sisemi tushikamane na mila sawa zikiwa nzuri au mbaya. Bali nimesema tushikamane na mila muda wa kuwa hatujaona mila zengine ambazo ni bora kuliko yetu aidha katika dini au dunia. Katika hali hiyo hakuna neno.

[1] 02:228

[2] 02:228

[3] 04:19

[4] 02:228

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (39) http://binothaimeen.net/content/888
  • Imechapishwa: 03/06/2020