Swali: Mwanaume anayeapa kutolala na mke kisha baadaye akalala naye anapaswa kutoa kafara? Ataitoa vipi?
Jibu: Atatakiwa kutoa kafara ya kuvunja kiapo, kwa sababu aliapa kuwa hatomwingilia. Atapomwingilia, basi amevunja kiapo chake. Uhalisia ni kwamba analazimika kuvunja kiapo hicho kisha atoe kafara.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
- Imechapishwa: 23/06/2023