Swali: Kuna mlinganizi katika nchi yetu anayetukana madhehebu ya Salaf-us-Swaalih na kusema kuwa al-Qaa´idah na ISIS ni mti[1] wa Salafiyyah na kusema kuwa kitabu “ad-Durar as-Saniyyah” ndio msingi wa ugaidi. Tunaomba utuwekee wazi?
Jibu: Huu ni upotevu. Huu ndio upotevu. Maneno haya ni ya kigaidi; kuwashtua watu na ulinganizi wa haki, ulinganizi wa Tawhiyd na Sunnah, kuwatuhumu tuhuma za uongo na kunasibisha mifumo ya mapote potofu na Ahl-us-Sunnah na kitabu “ad-Durar as-Saniyyah”. Ni uongo na uzushi. Huyu anataka kubatilisha ulinganizi katika Dini ya Allaah (´Azza wa Jall) na kuigeuza katika yale anayoyataka yeye kwa kuwapotosha watu na kuwafanya wayape mgongo madhehebu ya Salaf. Hakuna mafanikio isipokuwa kwa madhehebu ya Salaf. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hautofaulu watu wa mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyowafanya kufaulu wa mwanzo wao.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah huu utatofautiana katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Wakauliza: “Ni nani hao, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni yule mwenye kufuata yale niliyomo mimi leo na Maswahabah zangu.”

Huu ndio mfumo sahihi na ulio salama.

 [1] Tazama ISIS si kabisa mapando ya Salafiyyah – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Muhadharah%20%20-%206%
  • Imechapishwa: 07/02/2017