Swali: Kuwaita watu wa dini kwa ibara za mzaha kama kusema “gaidi” na “msimamo mkali”. Je, huku ni kufanya istihzai ambako kunapelekea katika matishio haya[1]?

Jibu: Bila shaka mtu kujiepusha na matamshi haya ndio jambo salama zaidi kwa mtu na kuitakasa dhimma yake. Haijuzu kufanya utani kwa mfano wa mambo kama haya. Ikiwa anamwita “gaidi” kwa sababu ya dini yake na kwamba dini ni ugaidi, huku ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Hata kama anafanya mzaha tu. Ama akiwa hakukusudia kuwa dini ndio ugaidi, bali anachokusudia ni mtu huyo yeye kama yeye na anamcheka, haya pasi na shaka ni maskhara. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ

“Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka wanaume wenzao, kwani huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wenzao, kwani heunda wakawa bora kuliko wao.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huenda mwenye nywele matifutifu anayefukuzwa milangonim lau atamuapia Allaah [amfanyie jambo fulani] angelimfanyia.”

Usimfanyie maskhara muislamu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/95-kitenguzi-cha-sita-mwenye-kufanya-istihzai-na-mambo-ya-dini/

[2] 49:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (06) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/06.mp3
  • Imechapishwa: 03/03/2019