Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya kazi ya kubadilisha pesa?

Jibu: Hapana vibaya kwa sharti ya kupeana mkono kwa mkono. Kubadilishana hakuna vibaya, lakini imeshurutishwa kupeana mkono kwa mkono. Wasitengane ilihali bado wanadaiana. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Muuzaji na mnunuzi bado wako na khiyari muda wa kuwa hawajatengana.”[1]

[1] al-Bukhaariy (2079) na Muslim (1532).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 03/07/2024