Swali: Mara nyingi nakosa swalah ya ´Aswr na naiswali nyumbani. Hilo ni kutokana na sababu ya kazi yangu ambayo inamalizika baada ya adhaana ya ´Aswr. Natoka kazini ilihali nimechoka. Sina wakati wa kupumzika na kula. Siwezi kuswali ndani ya wakati wake. Je, inasihi kwangu kuswali nyumbani kwangu na kuchelewesha swalah nje ya wakati wake?

Jibu: Uliyoyataja sio udhuru unaokujuzishia kuchelewesha swalah pamoja na mkusanyiko. Bali ni lazima kwako kuikimbilia pamoja na ndugu zako katika nyumba ya Allaah. Kupumzika na kula chakula iwe baada ya hayo. Allaah (Subhaanah) amekuwajibishia kuswali ndani ya wakati pamoja na ndugu zako katika mkusanyiko. Uliyoyataja sio udhuru wa kuichelewesha. Lakini hayo ni udanganyifu wa shaytwaan na nafsi inayoamrisha sana maovu, unyonge wa imani na uchache wa kumcha Allaah. Kwa hivyo tahadhari matamanio yako, shaytwaan na nafsi inayoamrisha sana maovu. Hivyo utakuwa na mwisho mwema na utafuzu kwa ukombozi na furaha duniani na Aakhirah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/379)
  • Imechapishwa: 01/10/2021