Swali: Mara nyingi napitwa na swalah na huikusanya na ambayo iko baada yake. Hilo ni kutokana na sababu ya uuguzi au kuwachunguza wagonjwa. Kadhalika huacha swalah ya ijumaa kwa sababu ya kuwahudumia wagonjwa. Je, kitendo changu hichi kinafaa?

Jibu: Ni lazima kuswali swalah ndani ya wakati wake. Haifai kwako kuichelewesha kutoka nje ya wakati wake.

Kuhusu swalah ya ijumaa, ukiwa mlinzi au mtu mfano wake miongoni mwa wale watu ambao hawawezi kuswali ijumaa pamoja na wengine, basi indondoka kutoka kwako. Badala yake utaiswali Dhuhr kama vile mgonjwa na wengineo.

Ama swalah nyenginezo ni lazima kuziswali ndani ya wakati wake. Haifai kwako kukusanya kati ya swalah mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/373)
  • Imechapishwa: 01/10/2021