Kauli mbili za wanachuoni juu ya kulipa Sunnah ya Fajr kwa iliyempita

Swali: Nikija kuswali swalah ya Fajr na nikamkuta imamu kishaanza kuswali na sikuwahi kuswali Sunnah ya Fajr. Je, niilipe baada ya swalah?

Jibu: Wanachuoni wana kauli mbili juu ya masuala haya. Wako ambao wanaona inafaa kuilipa baada ya swalah kwa sababu ni miongoni mwa mambo yenye sababu. Wako wengine wanaona kuwa hailipwi baada ya swalah lakini hata hivyo inalipwa wakati wa mchana kwenye Dhuhaa´. Kwa hiyo ukitaka kuilipa baada ya swalah ni sawa. Na kama unajiamini unaweza kuilipa wakati wa mchana katika Dhuhaa´ ndio bora na vyema zaidi kwa ajili ya kutoka nje ya tofauti. Lakini hata hivyo ukiilipa baada ya swalah hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (11) http://binothaimeen.net/content/6747
  • Imechapishwa: 28/11/2020