Ghunjar amesema: Muhammad bin ´Imraan al-Jurjaaniy ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad al-Bukhaariy akisema: Nimemsikia Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy akisema:

“Nimekutana na maelfu ya wanamme Hijaaz, ´Iraaq, Shaam na Misri na nimekutana nao mara nyingi. Nimekutana na watu wa Shaam, Misri na Jaziyrah mara mbili, watu wa Baswrah mara nne na Hijaaz miaka sita. Sikumbuki ni mara ngapi nilifika Kuufah na Baghdaad na wanachuoni wa Khuraasaan, akiwemo al-Makkiy bin Ibraahiym, Yahyaa bin Yahyaa, Ibn Shaqiyq, Qutaybah na Shihaab bin Ma´mar. Shaam nilikutana ikiwa ni pamoja na al-Firyaabiy, Abu Mushir, Abul-Mughiyrah na Abul-Yamaan. Sikumuona yeyote ambaye anaonelea tofauti kwamba: Dini ni maneno na matendo na kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/407-408)
  • Imechapishwa: 28/11/2020