Swali: Nikiingia ndani ya swalah punde kidogo kabla ya Rukuu´ ni jambo limesuniwa kusoma al-Faatihah au nisome du´aa ya kufungulia swalah? Imamu akirukuu kabla sijamaliza kusoma al-Faatihah nifanye kitu gani?

Jibu: Kusoma du´aa ya kufungulia swalah imependekezwa na kusoma al-Faatihah ni jambo la faradhi kwa maamuma kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni. Ukikhofia kwamba utakosa al-Faatihah basi anza nayo. Pindi imamu ataporukuu kabla hujaikamilisha basi rukuu pamoja naye na inakundondokea sehemu yake nyingine iliobaki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo imamu amewekwa ili afuatwe. Hivyo basi msitofautiane naye. Akisema “Allaahu Akbar” nanyi semeni “Allaahu Akbar” na akirukuu nanyi rukuuni.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] al-Bukhaariy (680) na Muslim (625).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/243)
  • Imechapishwa: 28/10/2021