Katika hali hii hakuna haja ya du´aa ya kufungulia swalah

Swali: Nikiingia msikitini na nikakuta imamu amerukuu au amesujudu – je, inafaa kwangu kusoma du´aa ya kufungulia swalah katika hali hii au inatosha du´aa ya imamu ya kufungulia swalah?

Jibu: Ukimkuta amerukuu au amesujudu basi lete Takbiyr na ujiunge naye. Katika hali hii hakuna haja ya du´aa ya kufungulia swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/24)
  • Imechapishwa: 28/10/2021