Swali: Je, inafaa kukata swalah ya mamkuzi ya msikiti kunapokimiwa swalah katika ile Rak´ah ya kwanza?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”[1]

Wanazuoni wamesema kuwa hiyo inafasiriwa ikiwa ni pale mwanzoni. Kwa msemo mwingine ameanza swalah na papohapo kukakimiwa swalah. Lakini kukikimiwa swalah baada ya kuinua kichwa chake kutoka katika Rukuu´ katika ile Rak´ah ya pili ya swalah iliyopendekezwa, basi anatakiwa kuikamilisha. Kwa sababu sehemu iliyobaki sio swalah kamili na hivyo hakuna neno.

[1] Muslim (710).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-يجوز-قطع-تحية-المسجد-إذا-أقيمت-الصلاة؟
  • Imechapishwa: 18/06/2022