Swali: Je, inajuzu kwa wanamme kutia hina mikononi na miguuni?

Jibu: Mwanamke ndiye anayepaka hina mikononi mwake kwa ajili ya kujipamba. Anaweka vilevile kichwani mwake. Lakini kuhusu mwanmme kupaka hina, ikiwa ni kutokana na haja ya kazi kwa sababu anafanya kazi ya muhunzi, seremala na mfano wake ambapo akalazimika kutia hina kwa sababu inamsaidia mikono yake kubeba vitu hivi, basi hakuna ubaya juu yake. Kwa sababu hiyo ni kwa lengo la kujikinga. Lakini akijipaka kwa lengo la kujipamba na kujifananisha na wanawake ni kitu kisichojuzu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/وضع-الحناء-في-اليدين-والرجلين-للرجال
  • Imechapishwa: 11/06/2022