Katika hali hii inajuzu kuishi katika miji ya makafiri

Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kuishi katika miji ya makafiri?

Jibu: Haijuzu kwake kuishi katika miji ya makafiri. Isipokuwa tu ikiwa kama hana uwezo wa kufanya Hijrah. Katika hali hii ni lazima kupatikane sharti ya kudhihirisha dini[1]. Inajuzu [kuishi katika miji ya makafiri] kwa sharti ikiwa kama hawezi kufanya Hijrah. Sharti ya pili adhihirishe dini yake. Katika hali hii itakuwa inajuzu kwa kiasi cha dharurah itavokuwa:

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

“Isipokuwa wale waliokandamizwa – kati ya wanaume na wanawake na watoto – ambao hawakuweza kupata namna yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah akawasamehe – Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria.” (04:98-99)

Lakini yule mwenye uwezo wa kufanya Hijrah haijuzu kwake kuishi katika miji ya makafiri:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao.” (04:97)

bi maana hawa ni wale waliokuwa wanaeshi katika miji ya makafiri.

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao [Malaika] watawaambia: “Mlikuwa katika nini?” (04:97)

bi maana mlikuwa sehemu gani.

قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ

“Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” (04:97)

bi maana hatukuweza kudhihirisha eini yetu.

قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

“[Malaika] watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni Motoni – na ubaya ulioje mahali pa kurejea!”

Ikiwa hawezi kudhihirisha dini yake na wakati huo huo ana uwezo wa kufanya Hijrah, basi katika hali hii itakuwa ni wajibu kwake kufanya hivo.

[1] Tazama Maana ya kudhihirisha dini katika miji ya kikafiri – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14705
  • Imechapishwa: 19/04/2015