Swali: Nina ami ambaye haswali na wala hamjui Allaah. Aidha anadai kwamba hamjui Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa mujibu wa maneno yake. Ninapomnasihi hunidhihaki na kunikejeli na kuniambia kuwa mimi ni mwendawazimu. Amenifukuza nyumbani kwa sababu yake. Nilipomwambia baba yangu aidha amchague mimi au yeye nyumbani, akaniambia kuwa mimi ndiye nitoke. Hali ya kuwa yeye ana nyumba yake mwenyewe. Mimi sitaki awaendeshe ndugu zangu kwa gari, khaswa kwa kuwa hajui dini. Ee Shaykh, ni ipi suluhisho pamoja naye na pia pamoja na familia yangu? Je, msimamo wangu nao ni sahihi hali ya kuwa sasa nimefukuzwa nyumbani?
Jibu: Hili ni jambo kubwa la uovu na mfano wa huyu ameritadi kutoka katika Uislamu na ukafiri mkubwa. Lakini ikiwa wewe ni mkweli, basi peleka jambo lake mahakamani, kwa wenye mamlaka au kwa wote wawili. Peleka kwa mahakama na kwa wenye mamlaka na uthibitishe mashahidi juu yake ili ahukumiwe kwa hukumu ya Allaah ambayo ni ima auawe au atakwe kutubia. Wala usinyamaze. Lakini usiwe peke yako. Tafuta watu wanaomjua miongoni mwa jamaa zako walio waaminifu na waadilifu, kwa sababu wanaweza kusema juu yako kuwa wewe ni mwongo na kwamba umezusha maneno haya baada ya wao kukufukuza. Lazima utafute watu wenye kuaminika; wawili, watatu au wanne washuhudie pamoja nawe mbele ya mahakama na mbele ya kiongozi wa mamlaka ili itekelezwe hukumu ya Allaah juu yake. Allaah akubariki, usinyamaze, si wewe wala wengine wanaowaona watu hawa. Mwenye kuwajua hawa wanaotukana dini, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufanya yanayopingana na Uislamu ni wajibu kuripoti jambo lao kwa mahakama na kwa wenye mamlaka katika nchi uliyomo. Lakini usiwe mmoja peke yako, mmoja haitoshi. Lazima utafute watu waaminifu pamoja nawe, mfuatilie mtu huyu, mjue matendo yake mabaya na maneno yake maovu ili jambo lake lipelekwe kwa ujuzi na ushahidi wa kundi ili wasikutuhumu kwa mambo usiyonayo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3399/كيف-التعامل-مع-من-يستهزى-بالدين-او-بالرسول
- Imechapishwa: 08/09/2026
Swali: Nina ami ambaye haswali na wala hamjui Allaah. Aidha anadai kwamba hamjui Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa mujibu wa maneno yake. Ninapomnasihi hunidhihaki na kunikejeli na kuniambia kuwa mimi ni mwendawazimu. Amenifukuza nyumbani kwa sababu yake. Nilipomwambia baba yangu aidha amchague mimi au yeye nyumbani, akaniambia kuwa mimi ndiye nitoke. Hali ya kuwa yeye ana nyumba yake mwenyewe. Mimi sitaki awaendeshe ndugu zangu kwa gari, khaswa kwa kuwa hajui dini. Ee Shaykh, ni ipi suluhisho pamoja naye na pia pamoja na familia yangu? Je, msimamo wangu nao ni sahihi hali ya kuwa sasa nimefukuzwa nyumbani?
Jibu: Hili ni jambo kubwa la uovu na mfano wa huyu ameritadi kutoka katika Uislamu na ukafiri mkubwa. Lakini ikiwa wewe ni mkweli, basi peleka jambo lake mahakamani, kwa wenye mamlaka au kwa wote wawili. Peleka kwa mahakama na kwa wenye mamlaka na uthibitishe mashahidi juu yake ili ahukumiwe kwa hukumu ya Allaah ambayo ni ima auawe au atakwe kutubia. Wala usinyamaze. Lakini usiwe peke yako. Tafuta watu wanaomjua miongoni mwa jamaa zako walio waaminifu na waadilifu, kwa sababu wanaweza kusema juu yako kuwa wewe ni mwongo na kwamba umezusha maneno haya baada ya wao kukufukuza. Lazima utafute watu wenye kuaminika; wawili, watatu au wanne washuhudie pamoja nawe mbele ya mahakama na mbele ya kiongozi wa mamlaka ili itekelezwe hukumu ya Allaah juu yake. Allaah akubariki, usinyamaze, si wewe wala wengine wanaowaona watu hawa. Mwenye kuwajua hawa wanaotukana dini, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufanya yanayopingana na Uislamu ni wajibu kuripoti jambo lao kwa mahakama na kwa wenye mamlaka katika nchi uliyomo. Lakini usiwe mmoja peke yako, mmoja haitoshi. Lazima utafute watu waaminifu pamoja nawe, mfuatilie mtu huyu, mjue matendo yake mabaya na maneno yake maovu ili jambo lake lipelekwe kwa ujuzi na ushahidi wa kundi ili wasikutuhumu kwa mambo usiyonayo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3399/كيف-التعامل-مع-من-يستهزى-بالدين-او-بالرسول
Imechapishwa: 08/09/2026
https://firqatunnajia.com/kamshtaki-baba-yako-mdogo-aadhibiwe/