74 – Abu Bakr bin Abiyn-Nadhwr ametukhabarisha: Abun-Nadhwr Haashim ametukhabarisha: Warqaa’ bin ´Umar al-Yashkuriy ametukhabarisha: Nimemsikia ´Ubaydullaah bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesimulia:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia chooni, nikamuwekea maji. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja, nikasema: ”Ni nani aliyefanya hivi?” Nikasema: ”Ibn ´Abbaas.” Ndipo akasema: ”Ee Allaah, mpe ufahamu!”[1]

75 – Muhammad bin Haatim ametukhabarisha: al-Qaasim bin Maalik ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik, kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniombea kwa Allaah mara mbili anipe hekima.”[2]

76 – ´Imraan bin Muusa ametukhabarisha: ´Abdul-Waarith ametuhadithia: Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, aliyesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinivuta kifuani mwake na kusema: ”Allaah, mfunze hekima!”[3]

[1] al-Bukhaariy (143) na Muslim (2477).

[2] at-Tirmidhiy (3823), aliyesema Hadiyth ni nzuri na ngeni. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3823).

[3] at-Tirmidhiy (3824), ambaye amesema Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3824).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 68-70
  • Imechapishwa: 08/09/2026