15. Fadhilah za al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib

70 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: ´Ubaydullaah ametukhabarisha, kutoka kwa Israa’iyl, kutoka kwa ´Abdul-A´laa, aliyeeleza kuwa amemsikia Jubayr akisema: Ibn ´Abbaas amenikhabarisha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”al-´Abbaas anatokana nami, nami natokana naye.”

71 – Humayd bin Makhlad ametukhabarisha: ´Aliy bin ´Abdillaah ametukhabarisha: Muhammad bin Twalhah at-Taymiy ametuhadithia: Naafiy´ Abu Suhayl ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib:

” al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib ndiye Quraysh mkarimu zaidi na anayeunga kizazi zaidi.”

72 – Zakariyyaa bin Yahyaa ametukhabarisha: Ishaaq ametuhadithia: Jariyr ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Hayyaan at-Taymiy – Yahyaa bin Sa´iyd bin Hayyaan –kutoka kwa Yaziyd bin Hayyaan, ambaye amesimulia:

”Mimi na Husayn bin Samurah bin ´Umar bin Muslim tuliondoka kwenda kwa Zayd bin Arqam na tukaketi kwake. Husayn akasema: ”Ee Zayd, tueleze kile ulichosikia na kukishuhudia kwa Mtume wa Allaah (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Akasema: ”Mtume wa Allaah (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama karibu na maji yanayoitwa Khumm. Akamuhimidi Allaah, akamsifu, akatoa mawaidha na kukumbusha kisha akasema: ”Enyi watu! Hakika mimi si jengine isipokuwa ni mtu. Nakaribiwa kujiliwa na mjumbe wa Mola wansgu na hivyo nimuitikie. Hakika nimekuachieni vizito viwili. Cha kwanza ni Kitabu cha Allaah. Ndani yake kuna uongofu na nuru. Yule mwenye kushikamana na kukishikilia barabara basi anakuwa juu ya uongofu, na yule mwenye kukiacha basi anakuwa juu ya upotofu. Na watu wa nyumbani kwangu; nakukumbusheni juu ya Allaah watu wa nyumbani kwangu.” Akasema hivo mara tatu. al-Huswayn akasema: ”Ni wepi watu wa nyumbani kwake, ee Zayd? Je, wakeze sio katika watu wa nyumbani kwake?” Akasema: ”Bali ndio, wakeze ni katika watu wa nyumbani kwake, lakini watu wa nyumbani kwake ni wale walioharamishiwa kupokea swadaqah.” Akasema: ”Ni kina nani?” Watu wa nyumbani kwa ´Aliy, watu wa nyumbani kwa ´Aqiyl, watu wa nyumbani kwa Ja´far na watu wa nyumbani kwa al-´Abbaas.”

73 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Abu ´Awaanah ametukhabarisha, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith: al-Muttwalib bin Rabiy´ah bin al-Haarith bin ´Abdil-Muttwalib amenihadithia:

”al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib aliingia kwa Mtume wa Allaah (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa amekasirika. Nilikuwa nyumbani kwake. Akasema: ”Ni kipi kilichokukasirisha?” Akasema: ”Ee Mtume, tuna nini sisi na Quraysh? Wanapokutana baina yao, basi wanakutana hali ya kuwa na nyuso zenye bashasha, na wanapokutana nasi, basi wanakutana nasi basi wanakutana nasi wakiwa kinyume na hivo.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakasirika sana mpaka uso wake ukapiga wekundu, na akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi Mwake! Imani ya mtu haingii ndani ya moyo wa mtu mpaka wakupendeni nyinyi kwa ajili ya Allaah na kwa ajili ya Mtume Wake.” Kisha akasema: ”Enyi watu! Yule mwenye kumuudhi ami yangu  basi ameniudhi mimi. Kwani hakika ami yake mtu ni kama baba yake.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (3758), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Mbali na jumla inayosema ”Kwani hakika ami yake mtu ni kama baba yake”

som sade att hadithen är god och autentisk. Frånsett meningen “En mans farbror är hans faders like” är hadithen svag enligt al-Albânî i “Dha´îf Sunan at-Tirmidhî” (3758).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 65-67
  • Imechapishwa: 08/09/2026