Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuniombea al–Wasiylah utamthubutikia uombezi wangu.”
Tunaomba utufafanulie maana yake.
Jibu: Hili limewekwa katika Shari´ah muumini baada ya adhaana. Anapoitikia muadhini, anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mnapomsikia muadhini, semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani anayeniswalia mara moja, basi Allaah humsifu mara kumi. Kisha muombeni Allaah anipe al-Wasiylah, kwani hiyo ni daraja katika Pepo. Haimstahikii isipokuwa kwa mja mmoja katika waja wa Allaah – na ninatarajia kuwa mimi ndiye huyo. Mwenye kuniombea al-Wasiylah, atahalalishiwa uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”[1]
Imekuka katika tamko jengine:
“Atapata uombezi.”
Hii al-Wasiylah ni daraja katika Pepo. Ni makazi makubwa katika Pepo kwa Nabii wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo inafaa kumuomba Allaah ampe daraja hii.
Imekuja katika tamko jengine:
“Mwenye kusema anaposikia adhaana:
اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ
“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi. Hakika Wewe huvunji ahadi.””[2]
Hii pia ni du´aa iliyopendekezwa baada ya adhaana. Ni kumuombea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Allaah ampatie al-Wasiylah, nayo ni daraja katika Pepo haistahiki isipokuwa kwa mja mmoja katika waja wa Allaah. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ninatarajia kuwa mimi ndiye huyo.”
Swali: Vipi uombezi wake Aakhirah?
Jibu: Uombezi wake unaombwa kwa Allaah. Yeye atauombea ummah siku ya Qiyaamah ili wahukumiwe na ili waumini waingie Peponi. Lakini unasema:
”Ee Allaah, mkubalie Nabii wako anishafie! Ee Allaah, nifanye miongoni mwa watu wa uombezi wake! Ee Allaah usininyime uombezi wake.”
Usiseme: “Ee Mtume wa Allaah nishafie” baada ya kufariki kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali muombe Allaah kwamba amkubalie kukuombea:
“Ee Allaah mkubalie Nabii wako anishafie! Ee Allaah nifanye miongoni mwa watu wa uombezi wake! Ee Allaah usininyime uombezi wake!”
Hivyo ndivyo muumini anavyomuomba Mola wake:
قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا
”Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah.”[3]
Ama katika uhai wake, hapana ubaya ikiwa yuko hai miongoni mwetu, kama ilivyokuwa kwa Maswahabah wake wakimuomba awaombee. Vivyo hivyo siku ya Qiyaamah watakapofufuliwa watu kutoka makaburini mwao na kukusanyika, waumini watamwendea na kusema:
“Ewe Mtume wa Allaah tuombee ili tuhukumiwe.”
[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] 39 :44
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3405/شرح-قوله-عليه-الصلاة-والسلام-من-سال-لي-الوسيلة
- Imechapishwa: 08/09/2026
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuniombea al-Wasiylah utamthubutikia uombezi wangu.”
Tunaomba utufafanulie maana yake.
Jibu: Hili limewekwa katika Shari´ah muumini baada ya adhaana. Anapoitikia muadhini, anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mnapomsikia muadhini, semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani anayeniswalia mara moja, basi Allaah humsifu mara kumi. Kisha muombeni Allaah anipe al-Wasiylah, kwani hiyo ni daraja katika Pepo. Haimstahikii isipokuwa kwa mja mmoja katika waja wa Allaah – na ninatarajia kuwa mimi ndiye huyo. Mwenye kuniombea al-Wasiylah, atahalalishiwa uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”[1]
Imekuka katika tamko jengine:
“Atapata uombezi.”
Hii al-Wasiylah ni daraja katika Pepo. Ni makazi makubwa katika Pepo kwa Nabii wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo inafaa kumuomba Allaah ampe daraja hii.
Imekuja katika tamko jengine:
“Mwenye kusema anaposikia adhaana:
اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ
“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi. Hakika Wewe huvunji ahadi.””[2]
Hii pia ni du´aa iliyopendekezwa baada ya adhaana. Ni kumuombea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Allaah ampatie al-Wasiylah, nayo ni daraja katika Pepo haistahiki isipokuwa kwa mja mmoja katika waja wa Allaah. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ninatarajia kuwa mimi ndiye huyo.”
Swali: Vipi uombezi wake Aakhirah?
Jibu: Uombezi wake unaombwa kwa Allaah. Yeye atauombea ummah siku ya Qiyaamah ili wahukumiwe na ili waumini waingie Peponi. Lakini unasema:
”Ee Allaah, mkubalie Nabii wako anishafie! Ee Allaah, nifanye miongoni mwa watu wa uombezi wake! Ee Allaah usininyime uombezi wake.”
Usiseme: “Ee Mtume wa Allaah nishafie” baada ya kufariki kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali muombe Allaah kwamba amkubalie kukuombea:
“Ee Allaah mkubalie Nabii wako anishafie! Ee Allaah nifanye miongoni mwa watu wa uombezi wake! Ee Allaah usininyime uombezi wake!”
Hivyo ndivyo muumini anavyomuomba Mola wake:
قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا
”Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah.”[3]
Ama katika uhai wake, hapana ubaya ikiwa yuko hai miongoni mwetu, kama ilivyokuwa kwa Maswahabah wake wakimuomba awaombee. Vivyo hivyo siku ya Qiyaamah watakapofufuliwa watu kutoka makaburini mwao na kukusanyika, waumini watamwendea na kusema:
“Ewe Mtume wa Allaah tuombee ili tuhukumiwe.”
[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] 39 :44
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3405/شرح-قوله-عليه-الصلاة-والسلام-من-سال-لي-الوسيلة
Imechapishwa: 08/09/2026
https://firqatunnajia.com/makusudio-ya-al-wasiylah-katika-hadiyth-ya-kumuikia-muadhini/