adh-Dhahabiy amesema katika “Miyzaan-ut-I´tiqaad” wakati alipokuwa anaandika wasifu wa al-Haarith al-Muhaasibiy:
“Haafidhw Sa´iyd bin ´Amr al- Barda´iy amesema: “Nilikuwa na Abu Zur’ah wakati alipoulizwa kuhusu al-Haarith al-Muhaasibiy na vitabu vyake. Akamjibu muulizaji: “Ninakutahadharisha na vitabu hivi. Vina Bid´ah na upotevu. Shikamana na mapokezi. Humo kuna yakutosheleza kwako.” Kukasemwa: “Kuna mafunzo ndani yake.” Akasema: “Asiyekuwa na mafunzo katika maandiko ya Allaah hana mafunzo yoyote katika vitabu hivi.”
al-Haarith amekufa 243. Ni nani ambaye anaweza kulinganishwa na al-Haarith? Jifikirie lau Abu Zur´ah angeliona vitabu hivi vya mwishoni kama “al-Quut” cha Abu Twaalib. Ni kitabu gani kinaweza kulinganishwa na al-Quut? Jifikirie lau angeliona kitabu cha Ibn Jahdham “Bahjat-ul-Asraar” na kitabu cha as-Sulamiy “Haqaaiq-ut-Tafsiyr”. Angelipoteza akili yake. Jifikirie lau angeliona vitabu vya Abu Hamiyd [al-Ghazaaliy] at-Twuusiy na zile Hadiyh nyingi za kuzushwa zilizko kwenye “al-Ihyaa´”. Jifikirie lau angeliona kitabu cha Shaykh ´Abdul-Qaadir “al-Ghunyah”. Jifikirie lau angeliona [vitabu vya Ibn ´Arabiy] “Fusuus-ul-Hikam” na “al-Futuuhaat al-Makiyyah”. Wakati al-Haarith alikuwa katika kipindi ambacho kuliwepo uzungumzaji kulikuwepo maelfu ya maimamu katika Hadiyth ikiwa ni pamoja na Ahmad bin Hanbal na Ishaaq bin Raahuuyah. Wakati maimamu walipokuwa watu kama Ibn-ud-Dakhmiysiy na Ibn Shahaanan walikuwa wakiwaonelea kuwa ni wanachuoni wakubwa Allaah akiwa watu kama mwandishi wa “al-Fusuus” na Ibn Sufyaan. Tunamuomba Allaah afya na msamaha.”[1]
Jifikirie lau Abu Zur´ah, adh-Dhahabiy na wanachuoni wengine wakubwa wangeliona vitabu vya Sayyid Qutwub ambavyo ndani yake mna Huluul, umoja wa dini na uhuru wa dini. Vitabu ambavyo ´Adnaan ´Ar´uur anavipa kipaumbele na ambavyo mwandishi ni mtetezi wa Abul-Hasan al-Ma´ribiy. Watu wote hawa wawili wanatetewa na kusifiwa na ´Aliy bin Hasan al-Halabiy.
Jifikirie lau wangelimuona jinsi Abul-Hasan anavyowatetea wale wanaoita katika umoja wa dini, uhuru wa dini na udugu wa dini.
Jifikirie lau wangelimuona jinsi ´Aliy al-Halabiy alilazimisha gazeti ambalo lilikuwa na umoja wa dini, udugu wa dini, uhuru wa dini na upotevu mwingine na kuonelea kuwa linauwakilisha Uislamu na ukati na kati.
Jifikirie lau angeliona jinsi wanavyowatetea Ahl-ul-Bid´ah na kuwazingatia kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah.
Jifikirie lau wangeliona jinsi wanavopiga vita dhidi ya Ahl-us-Sunnah na wanasema kuwa ni wepetukaji mipaka, wamepinda, Khawaarij na kadhalika.
Jifikirie lau wangeliona jinsi wanavyobuni kanuni ili kutetea upotevu na kupiga vita dhidi Ahl-us-Sunnah.
[1] 1/431
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan maa fiy Naswihati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 70-71
- Imechapishwa: 27/08/2020

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan maa fiy Naswihati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 70-71
Imechapishwa: 27/08/2020
https://firqatunnajia.com/jifikirie-lau-abu-zurah-na-adh-dhahabiy-wangelimuona-qutwub-aruur-al-maribiy-na-al-halabiy/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)