Unatakiwa kutangaza sababu za mgawanyiko wa vijana wa Salafiyyuun na wale waliosababisha hilo ili baada ya hapo uweze kufikisha haki na kuwatunza wale ambao wamewaganya vijana na kuzusha kanuni zisizokuwa za salama ili kuwatetea Ahl-ul-Dhwalaal wal-Bid´ah. Kukosoa kanuni zao zisizokuwa za salama na misingi, mifumo ya kipotevu, kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal, vita dhidi ya Ahl-us-Sunnah na kuvuruga mfumo wao na wanachuoni.

Ungeliwataja wapekutevu na waasi waliokuza fitina na khatari yake. Wamesababisha fitina hii na wamepuliza maisha ndani yake kwa njia zao danganyifu na kanuni batili. Wamezitunga ili kuharibu mfumo wa Ahl-us-Sunnah na kuwapindua wanachuoni wake. Watu wengi wamedanganyika na njia hizi danganyifu, vilio vya kujifanyisha na kanuni batili ambazo lengo lake ni kuraddi haki na kuwapotosha viumbe. Fitina imekuwa kubwa zaidi na khatari kwa watu hawa. Matokeo yake imefanya Ahl-us-Sunnah wengi wamepotea. Wengi wameogopa baada ya kuwa walikuwa njiani wakielekea huko. Bila ya shaka inajulikana ni kina nani walio nyuma ya fitina na mgawanyiko huu katika Da´wah ya Salafiyyah…

Wanachuoni ndio warithi wa Mitume katika nasaha hii, mashauriano na mengineyo.

Pamoja na kwamba ilani yako haiishi katika masharti yake kwa mtazamo wa Kiislamu, ninaonelea kuwa ni wajibu juu yangu kukamilisha yale yaliyo na manufaa kwa Uislamu na Waislamu. Kwa ajili hiyo ninasema kwamba viongozi, watungaji na wachocheaji wa fitina hizi wanajulikana kwa Ahl-us-Sunnah wenye akili. Ni ´Adnaan ´Ar´uur, Abul-Hasan al-Ma´ribiy, ´Aliy al-Halabiy na wale wenye kuwafuata na kushikamana na kanuni na mfumo wao. Watu hawa wanawapiga vita Ahl-us-Sunnah na wanawatetea Ahl-ul-Bid´ah wakubwa. Wanapita kwenye njia ya mmisri freemason mkubwa Muhammad ´Abduh na mwanafunzi wake Jamaal-ud-Diyn al-Qaasimiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan maa fiy Naswihati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 9-10
  • Imechapishwa: 27/08/2020