Masuala haya ni makubwa sana ambayo kunapewa mtihani kati ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na watu wa Bid´ah na wapotevu. Anayekanusha Allaah kuwa juu, basi huyu ni katika wapotevu na wapindaji. Bali kuna wanachuoni ambao wamemkufurisha mwenye kufanya hivo kwa sababu anapinga kitu kimechothibitishwa na dalili za Qur-aan na Sunnah. Kuna dalili nyingi sana juu ya hilo. Sifa ya ujuu ni sifa ilio wazi kabisa. Anayepinga ujuu ni mwangamivu na ametenda Bid´ah mbaya sana. Kunachelea juu yake akawa ni mwenye kumkufuru Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 27/08/2020