Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni katika Sunnah kuwakata Ahl-ul-Bid´ah na kujiweka nao mbali, kuacha mjadala, ugomvi katika dini, kutosoma vitabu vya watu wa Bid´ah. Kutosikiliza maneno yao na kila jambo jipya katika dini ni Bid´ah na kila mwenye kujiita kwa kitu kingine zaidi ya Uislamu na Sunnah ni mzushi, kama mfano wa Raafidhwah, Jahmiyyah, Khawaarij, Qadariyyah, Murji-ah, Mu´tazilah, Karraamiyyah, Kullaabiyyah na mfano wao. Haya ni mapote ya upotofu na vipote vya Bid´ah, Allaah atukinge navyo.”

Haya ndio ambayo yalikuwa yakiusiwa na maimamu wa Ahl-us-Sunnah wako nashitu na watu wa Bid´ah sawa iwe katika vikao vyao na kuchanganyika nao. Kinachotakiwa ni kuwakata kwa maneno na viwiliwili ili Bid´ah na shari yao isiweze kuenea.

Kutangamana na kukaa na mtu wa Bid´ah, sawa iwe ni Bid´ah kubwa au ndogo, kunyamazia hilo, kutowasusa, kufanya nao anasa na kutowaraddi ni msimamo wa wapotevu.

Ahl-us-Sunnah wamejitofautisha kwa kuwa na msimamo imara ambapo wanawafanyia ukali na ugumu Ahl-ul-Bid´ah. Haijalishi ni Bid´ah ipi. Ahl-us-Sunnah wanawasusa Ahl-ul-Bid´ah. Jambo hili ni katika mambo ya misingi ya Uislamu, bali ni katika mambo ya msingi wa Sunnah. Aina ya Bid´ah ni khatari zaidi kuliko dhambi kubwa. Bid´ah ni mbaya na khatari zaidi kuliko dhambi kubwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 27/08/2020