Je, wafuasi wa makundi potofu wanapewa udhuru?

Swali: Je, wale wafuasi wa madhehebu ya Shiy´ah wanapewa udhuru kwa ujinga wao?

Jibu: Wanaweza kupewa udhuru kwa namna ya kutokufurishwa isipokuwa baada ya kubainishiwa. Hata hivyo hawapewi udhuru katika kufuata batili. Wanatakiwa kufunzwa na kuelekezwa. Isitoshe wanastahiki kususwa mpaka wajirejee kunako ile batili waliyomo. Kuhusu kukufurishwa pengine wakapewa udhuru kwa njia ya kutokukufurishwa mpaka wabainishiwe kwanza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23996/هل-يعذر-عوام-الشيعة-بجهلهم
  • Imechapishwa: 15/08/2024