Kuhusu wasabai, wako waliosema kuwa ni aina fulani ya manaswara. Wengine wakasema kuwa ni wale ambao hawana dini. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئِينَ وَالنَّصَارَىٰ وَالْمَجُوسَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا إِنَّ اللَّـهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ

“Hakika wale walioamini, na ambao mayahudi na wasabai na manaswara wa waabudia moto na wale wanaoshirikisha; hakika Allaah atahukumu kati yao siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.”[1]

Hizi ni dini sita.

Kimsingi neno sabai ni yule asiyekuwa na dini. Ni wale waliotoka nje ya dini za Mitume. Kuna wengine pia wamesema kuwa wako wasabai wapwekeshaji na wasabai makafiri. Huu ndio udhahiri wa mambo. Wako wasabai ambao ni waumini ambao ni katika watu wa Kitabu. Ni vipi basi watu hawa watakuwa ni wajuzi zaidi juu ya Allaah, Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuliko Salaf wa ummah?

[1] 22:17

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 13/08/2024