Swali: Kuna mmoja wao alosema kuhusu Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) ya kwamba ana chembechembe za Takfiyr.

Jibu: Hili halikusemwa juu ya Imaam al-Barbahaariy peke yake. Limesemwa juu ya maimamu wote wa Ahl-us-Sunnah ya kwamba ni Takfiyriyyuun. Wamesema pia kuwa Imaam Ahmad ni Takfiyriy kwa kuwa anaonelea asiyeswali ni kafiri. Wamesema haya kwa asiyekuwa al-Barbahaariy. Watu hawa wapuuzwe kwa kuwa wanataka watu wawe juu ya yale waliyomo na kusiwe na mambo yenye kutengua Uislamu. Wanasema kuwa hakuna mambo yenye kuvunja Uislamu na kwamba watu wako wako sawa sawa. Mwenye kusema ´mimi ni muislamu` anakuwa muislamu hata kama hatoswali na kufanya atakayo katika mambo yanayovunja Uislamu bado atakuwa ni Muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-9.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020