Peponi kutakuwa ´ibaadah?

Swali: Je, kumethibiti kitu katika Sunnah kuonyesha ya kwamba watu wa Peponi hawatofaradhishiwa mambo ya ´ibaadah kama mfano wa Swalah, Swawm na mengineyo?

Jibu: Pepo ni Nyumba ya malipo na sio Nyumba ya matendo. Pepo ni Nyumba ya malipo peke yake na sio Nyumba ya matendo. Hakuna matendo kama ambayo yapo [hapa] duniani. Kwa kuwa matendo yameisha duniani na kilichobaki ni malipo tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020