Je, mwanamke anaweza kutoa adhaana na kukimu?

Swali: Je, mwanamke anawajibika kutoa adhaana na kukimu wakati wa swalah?

Jibu: Hapana, si wajibu kwake adhaana wala kukimu. Wewe umesema “Je, anawajibika?”, kuna tofauti kati ya kusema “Je, anawajibika?” na “Je, anaweza?”, hio ya kwanza maana yake ni “Je, anawajibika kufanya hivyo?”, tofauti ungesema “Je, anaweza?” – kwa maana “Je, imependekezwa?”. Jibu ni kutokana na kadiri ya swali lako (ulivyokusudia), hawajibiki.

Lakini akiadhini na kukimu itakuwa jambo zuri, kama alivyosema ´Allaamah Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake al-Mughniy. Akitoa adhaana na akakimu ni jambo zuri na imependekezwa. Na ikiwa hatofanya katika swalah ya faradhi bila ya kutoa adhaana wala kukimu, swalah yake ni sahihi; akipatia sharti za swalah, nguzo zake na wajibu wake.

Ama Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) yeye anaona asiadhini wala asikimu.

Na kauli ya Ibnu Qudaamah In Shaa Allaah ndio yenye nguvu, ya kwamba akitoa adhaana na akakimu hakuna ubaya. Na ikiwa hatofanya hana juu yake kitu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=2048
  • Imechapishwa: 26/08/2020